November 28, 2015

 
Alfonce Mawazo enzi za Uhai wake
Viongozi wa Kitaifa wa Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), leo wamewaongoza mamia ya wakazi wa mkoa wa Mwanza kutoa heshima za mwisho, za kuuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoa wa Geita Marehemu Alphonce Mawazo.

 

Katika shughuli hiyo baba mdogo wa Marehemu Alphonce Mawazo, Charles Lugiko na mtoto mkubwa wa Marehemu Prescious Mawazo wakatoa ujumbe mzito, huku mwanaye anayesoma darasa la nne akiahidi kuwa siku moja atarithi mikoba ya baba yake katika ulingo wa Siasa.

 

 
Aliyekuwa Mgombea Urais wa CHADEMA na kupeperusha bendera ya UKAWA, Mhe. Edward Lowassa akitoa salamu zake za mwisho kwa aliyekuwa M/kiti CHADEMA moa wa Geita Alphonce Mawazo aliyeuwawa kikatili kwa kukatwakatwa mapanga 

Safari ya kuusindikiza Mwili wa Marehemu Alphonce Mawazo, imeanzia hapa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando Jijini Mwanza, ambapo mwili wake ulihifadhiwa kwa kipindi cha siku takribani kumi na nne, tangu mahuti hayo yalipomkuta Novemba 14 mwaka huu.

 

Kituo cha kwanza cha safari hii kikawa nyumbani kwa baba yake mdogo kata ya Luchelele Nyegezi eneo la Sweya, ambapo taratibu mbalimbali za kifamilia zimefanyika, kabla ya kuanza safari ya kuupeleka mwili wake katika viwanja vya Furahisha kwa ajili ya kuagwa.

 

 

Mwenyekiti CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe akitoa salamu za mwisho kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Mkoa wa Geita kamanda Alphonce Mawazo ambaye ameagwa kitaifa katika Viwanja vya Furahisha jijini Mwanza
 

Taratibu hizo zilipokamilika safari ya kuelekea katika viwanja vya Furahisha Jijini Mwanza ikawadia, ambapo katika viwanja hivyo viongozi wa Kitaifa wa (Chadema) wakaungana na mamia ya wakazi wa mkoa wa Mwanza kutoa heshima za mwisho.
 
Baada ya shughuli hiyo wafuasi wa Chama hicho wakaungana katika safari ya kuusindikiza mwili wa Marehemu Alphonce Mawazo, hadi mkoani Geita ambako utahifadhiwa katika Hospitali ya wilaya hiyo, kwa ajili ya kuagwa siku ya Jumapili katika viwanja vya Magereza.
 
Shughuli hiyo itakapokamilika Mwili wake utapelekwa katika mji mdogo wa katoro, ambako aligombea Ubunge wa Jimbo hilo kwa ajili ya kuagwa, kabla ya safari ya kuelekea Kijijini kwao kata ya Chikobe, ambako mazishi yatafanyika siku ya Jumatatu majira ya saa nne asubuhi.
  
 Familia ya Marehemu Alphonce Mawazo wakiendeshwa na mchungaji kwa ibaa fupi iliyofanyika nyumbani kwa baba Mdogo wa Marehemu.
  
Mwili wa marehemu Alphonce Mawazo ikiwasili nyumbani kwa baba mdogo (Charles Lugiko) Nyegezi jijini Mwanza ukitokea Hospital ya Bungando kwaajili ya ibada fupi
  

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE