September 25, 2015

 

Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizokumbwa na taharuki kubwa baada ya jana kutolewa kwa taarifa ya vifo vya mahujaji vilivyotokea huko Saudi Arabia.

Taarifa iliyotolewa na Mufti Mkuu wa Tanzania aliyeko huko Sheikh Abubakar Zuber zimesema miongoni mwa waliopoteza maisha ni pamoja na Watanzania watano na mmoja wao ni Raia wa Kenya.
Amewataja majina yaliyoweza kutambulika kuwa kuwa ni Bi Mwanaisha Juma,Mkungwe Suleiman na Seif Said.
Amesema katika kipindi hiki wanaendelea kufanya mawasiliano na Wizara husika wakishirikiana na ubalozi wa Tanzania kupata taarifa za kina na amewaondoa hofu na kuahidi kurtoa taarifa zenye ukweli.
Kutokana na idadi kubwa ya maiti serikali ya Saudi Arabia inaendelea na zoezi la kutambua uraia wa kila mwili na kutoa taarifa kwa nchi husika. 

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE