August 29, 2015

Mamlaka ya udhibiti wa chakula na dawa TFDA kanda ya kati imeteketeza  vinywaji baridi,vipodozi na madawa ambayo yamekwisha muda wake,yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni saba,ambayo yalikamatwa yakiuzwa katika maeneo mbalimbali ya manispaa  ya Morogoro.

Hatua hiyo ya uteketezwaji wa bidhaa imekuja baada ya TFDA kanda ya kati kufanya ukaguzi katika maduka ya vinyaji baridi,vipodozi na madawa katika kata tano za manispaa ya Morogoro na kubaini na kuzikamata bidhaa mbalimbali zilizokuwa zikiuzwa wakati zimewisha muda wake  wa matumizi,ambapo mkaguzi wa  TFDA kanda ya kati, Abel  deule,amesema bidhaa hizo zilikuwa zikiuzwa na kutumika kinyume na sheria na kusababisha madhara makubwa ya kiafya ikiwemo saratani kwa watumiaji,athari kubwa zikiwa ni kwa wanawake na watoto.

Nao wananchi wamesema hatua iliyochukuliwa na TFDA ni nzuri na fundisho kwa wafanya biashara wanaokiuka sheria kwa kuuza bidhaa zilizopitwa na wakati,kwa kuangalia  zaidi maslahi yao kuliko kujali afya za watumiaji ambao ni wateja wao.
Kuteketezwa kwa bidhaa hizo kumekuja wiki mbili tu tangu TFDA kanda ya kati,kuyafungia machinjio ya nyama katika manispaa ya Morogoro kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kukithiri kwa uchafu na uchakavu na kutotumika kwa baadhi ya miundo mbinu.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE