Bongo
Fleva mwaka huu inaweza kumake headlines zaidi kisiasa kama
waliotangaza nia wakafanikiwa kushika nafasi hizo wanazoziomba kutoka
kwa Watanzania,kuna waliotangaza kugombe Ubunge na wapo waliotangaza
kugombea nafasi za Udiwani.
Fid Q alifikiwa na mic ya millardayo.com
kutaka kufahamu kama nae ana mpango wowote wa kujiunga na
siasa>>’Sijioni kuwa Mwanasiasa ingawa takribani miaka 4 iliyopita
na kila siku nakutana na watu wananiambia kuwa nafaa kuwa Mwanasiasa
kutokana na uwezo wangu wa kuchanganua mambo ‘
Kwenye sentensi nyingine Fid Q
amesema >’Kinachonishinda kwenye siasa kuna siku nilijifunza
mapinduzi ni kitu kinachoendelea,tunakaa mtaani tunaimba Malaria mara
inakuja Dengue,tunaimba kuhusu mafuriko mara yanakuja mabomu na
serikalini kupo hivyo unaingia ndani unakuta kuna mapengo kibao kwa hiyo
utaamua mwenyewe kama utakua mkweli au lah na ukitaka kuwa mjuaji sana
kuna matatizo yake pia’
Sentensi ya mwisho ya Fid Q ameimaliza
kwa kusema >>’Nachokiogopa ni kuwa Mwanasiasa nipate zile hela
nyingi halafu nianze kuwa wa uongo hicho ndicho kinachonitisha lakini
sioni kama siasa inanishinda naogopa uongo wa siasa’.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment