May 25, 2015

 
 Waziri Mkuu aliyejiuzulu Edward Lowassa.
WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu Edward Lowassa amesafirisha wahariri wakuu wa vyombo vyote vya habari toka Dar es salaam na kufanya nao mkutano maalum leo nyumbani kwake mjini Dodoma. Katika mkutano huo kwa ufupi Lowassa amesema yafuatayo;

1: Amesema Hahusiki lolote na sakata la Richmond na ndio sababu hata kamati ya Mwakyembe haikuona sababu ya kumhoji. Amesisitiza kuwa cheo cha uwaziri mkuu ndio ilikuwa lengo la kamati ya mwakyembe na spika wa bunge kipindi hicho Samwel Sitta. Amesisitiza hicho sio kikwazo kwake katika kuingia Ikulu kwani sakata la Richmond lilipikwa kumchafua. Amechukua muda mrefu kuzungumzia hili la Richmond na amesema atalisema zaidi Arusha wikendi hii.
2. Anaamini kila mtangaza nia ana makundi ya kumuunga mkono. Yeye katika mkutano huu na wahariri leo ameambatana na Nazir Karamagi, Peter serukamba, Diana chilolo, Hussein Bashe na wengineo huku wengi wakiwa ni waliojeruhiwa katika serikali ya awamu ya nne akiwemo Aliekuwa DC Igunga Elibariki Kingu. Pia aliekuwa mkurugenzi wa HakiElimu Elizabeti Misoki ametangazwa rasmi kuwa Mkurugenzi wa mahusiano na mawasiliano katika timu ya kampeni ya Lowassa. Amehoji kwani akina karamagi wana tatizo gani na kwani wao sio binadamu?
3. Lengo kuu atakaloanza nalo ni Elimu na sio Kilimo kwanza cha serikali ya JK. Amesema serikali ya JK ilikosea kuanza na kilimo na kuweka kando elimu. Ametangaza kuwa sera yake ni Elimu Kwanza.
4. Kuhusu pesa anasema anapata michango ya rafiki zake na ataendelea kupokea michango hii wakati wote wa harakati zake na haina madhara yotote.
5. Anasema hatahama CCM na asiemtaka yeye CCM ndie aondoke ndani ya chama kwani yeye ana uhakika wa kupata nafasi kuwania urais.
6. Amesema hatalipa kisasi kwa lolote lililomtokea katika siasa. Amemwachia Mungu kwani yeye ni mcha Mungu.
7. Amesema Arusha itawaka moto tarehe 30 mwezi huu na kuwataka watanzania kutega sikio kwani ataanika kila jambo kuhusu mustakabali wa nchi hii na mipango yake ya kuiinua nchi kiuchumi katika miaka kumi ijayo.
Hayo ni kwa ufupi. Wahariri wakuu katika media zote kupitia Jukwaa la Wahariri walikuwepo, na Absalom Kibanda na Nevil Meena ndio walikuwa waratibu wakuu wa mkutano huu.
CHANZO: JAMII FORUM

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE