January 23, 2015

 
 Wafugaji jamii ya wamasai na wabarabaigi mkoani Morogoro wamefunga minada yote ya kuuza mifugo mkoani Morogoro kwa muda usiojulikana wakilalamikia serikali kushindwa kukomesha vitendo vya uonevu wanavyofanyiwa na madereva wa  bodaboda kwa kupigwa na kufukuzwa kila wanapongia katika mji wa morogoro.
 

Wakizungumza kwenye mkutano uliojumuisha wafugaji kutoka wilaya za Morogoro, Gairo Mvomero na Kilosa wakiwa na viongozi wao wakuu wa jadi wanaofahamika kama malaigwenani wafugaji hao wameazimia kufunga minada yote kwa muda usiojulikana.
Mbali na maamuzi hayo wafugaji hao pia wameazimia kuacha kuuza maziwa na mifugo  mkoani Morogoro na watakaobainika kukiuka  agizo hilo watalipishwa faini ya shilingi milioni moja hadi hapo serikali  itapoamua kuingilia kati  migogoro ya wakulima na wafugaji.
Katika hatua nyingine kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Morogoro imetembelea kijiji cha Mabwegele kujionea athari za watu kuchomewa nyumba ambapo mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt Rajab Rutengwe amesema serikali haitasita kuchukua hatua kwa waliohusika na tukio hilo, na tayari wizara ya ardhi nyumba na maendeleo ya makazi imemteua Bw  Paul Kimiti  kufika mkoani hapa kufanya usuluhishi  kwa lengo la kumaliza migogoro hiyo.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE