January 22, 2015

Rais wa TZ kulifanyia mabadiliko Baraza la Mawaziri 
 Mawaziri wote wa baraza la mawaziri nchini Tanzania wamezuiwa kusafiri kikazi nje ya Jiji la Dar es Salaam kutokana na kile kinachoelezwa ni maandalizi ya kukabidhi ofisi kwa mawaziri wapya ambao wanatarajiwa kutangazwa wakati wowote kuanzia sasa. Taarifa hizo zimekuja siku moja tu tangu Ikulu kupitia kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Salvatory Rweyemamu, kuwataka Watanzania kuwa na subira kwa kuwa Rais Jakaya Kikwete wakati wowote kuanzia sasa atatoa uamuzi dhidi ya tuhuma zinazomkabili Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo. Profesa Muhongo na baadhi ya viongozi wengine wa Serikali,
wanahusishwa na sakata la uchotwaji wa zaidi ya Sh bilioni 300 kwenye akaunti ya Tegeta Escrow. Taarifa zaidi zinasema kuwa, mawaziri wote sasa wamezuiwa kusafiri nje ya Dar es Salaam kutokana na kusubiri mchakato huo wa kukabidhi ofisi. Vyanzo hivyo viliongeza kwamba tayari Rais Kikwete amekwishamaliza mchakato wa uteuzi wa baraza jipya la mawaziri, akiwa nchini Uswisi katika Mkutano wa Jukwaa la Uchumi la Dunia. Mrengo wa upinzani nchini Tanzania umekuwa ukisisitiza juu ya kufutwa kazi mawaziri wote waliohusika katika sakata la Escrow.

Chanzo:idhaa ya kiswahili Iran

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE