January 24, 2015

Tangazo la mfalme mpya wa Saudi Arabia, Salman, Januari 23 mwaka 2015 mjini Riyad. 
 Salman bin Abdulaziz al-Saud, ndugu wa Abdullah na mtoto wa mwanzilishi wa ufalme, hatimaye ni mfalme wa Saudi Arabia na mlinzi wa maeneo mawili takatifu ya Uislamu.

 Ijumaa, Januari 23, baada ya kutangazwa kifo cha Abdullah, mfalme Salman aliitisha mara moja kikao cha Baraza la utawala wa kifalme na kuteuliwa ndugu yake mwingine, Moqren, kama mrithi wake.
Wakati huo huo mfalme Salman ameongea kwenye televisheni ya taifa akihakikishia ulimwengu na raia wa Saudia mwendelezo wa utawala wa kifalme na sera zake.
Katika hotuba yake ya kwanza ya mfalme, Salman wa Saudi Arabia, mwenye umri wa miaka 79, amethibitisha kwamba hakutakuwa na mabadiliko katika siasa za nchi.
" Sisi tutakaa na nguvu ya Mungu, kwenye njia ya haki ambayo taifa hili lilifuata tangu kuanzishwa kwake na mfalme Abdul Aziz bin Saud na wanawe baada yake", amesema mfalme Salman.
" Mungu alitaka mimi nipewe majukumu haya makubwa, naomba kwa Mungu anipe msaada huo", ameongeza mfalme Salman.
Saudi Arabia ni nchi ya kwanza kwa uzalishaji wa mafuta. Uzalishaji wake wa dhahabu nyeusi unalinda ushawishi wa shirikisho la la nchi zinazouza mafuta (Opep). Saudi Arabia pia ni mchangiaji muhimu katika mahusiano na Mashariki ya Kati, hasa katika miaka ya hivi karibuni. Riyadh ni mshirika muhimu wa Marekani na nchi za Magharibi katika sekta ya kidiplomasia.
Serikali ya Saudi Arabia ina mwelekeo wa Kiislamu. Mfalme mpya ametoa wito kwa umoja miongoni mwa Waislamu ambao wamegawanyika kutokana na vita vinavuendelea duniani.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE