January 23, 2015

   

 Muigizaji Lulu Michael ambae ambaye kwa sasa bado anatamba na movie yake ya 'Foolish Age' amefunguka na kuonyesha hisia zake za ndani kwa mwanamuziki
 
Marlaw ambae alishawahi kutamba na hits song kibao zikiwepo Bembeleza,Rita,na missing my baby (Pipii).
Lulu ameonyesha hisia zake hizo kupitia ukurasa wake wa Instragram ambapo anajaribu kujiuliza maswali kuhusu kupotea kwa mkali wa Bongo fleva ambae alitamba sana na kuweza kufanikiwa kushika watu kutokana na uwezo wake kisanaa.
Lulu Michael anajaribu kujiuliza nini kilimkuta au nini kimemfanya Marlaw kuwa kimyaa kisanaa ili hali uwezo wake ulikuwa mkubwa sana maana hakubana pua wala hakusingiziwa lakini alifanya vizuri,Lulu anajiuliza tulimkosea nini msanii huyu.
"Kwani tulikukosea nn kaka!??? mbona ukatuonjesha na kutuondolea burudani tena!??? i believe ur talented tena sio kidogo, sio kwa kubana pua, sio kwa kusingiziwa, pengine majukumu Ya ki kazi Au Ya kifamilia yamebana Lakini naamini u have something to offer the whole world....Rudi msaidiane kuendelea kupeleka mziki unapotakiwa kufika Jamanii.!
Msanii Marlaw ambae kwa sasa ni baba wa familia na mwenye mtoto mmoja na msanii mwenzake Besta alikaririwa mwaka jana na vyombo mbalimbali vya habari kuwa anajipanga ili aweze kutoa kazi kuwaridhisha mashabiki wake ambao wamekuwa waki miss kazi zake.
katika hili Lulu anaamini kuwa kutokana na uwezo alionao Marlaw akirudi katika tasnia ya muziki tena akisaidiana na wenzake ambao kwa sasa wameanza kufanya vizuri katika tasnia ya muziki Afrika ingesaidia kukuza muziki wa Bongo flvea nakufika mbali zaidi kutokana na uwezo wao katika sanaa.
Katika kufikisha kilio chake kwa mwanamuziki huyo Actress Lulu amemaliza kwa kusema kuwa yeye ni shabiki mkubwa sanaa wa kazi na anajua sanaa kuimba.
"I'm a fan...a big fan????????unajua sana yani"
Mbali na hao mashabiki pia wameungana na Lulu kufikisha kilio chao kwa mwanamuziki Marlaw kwa kusema haya
Athumanalmas Kweli kabsa unayosema mdg wng Lulu,kijana anatkiwa arudshe heshma ya mziki wake
Janethrain35 Lulu umenikumbusha mbali sana we miss him so very much
Veronicapius Uyo jamaa ni shida sana enzi nipo xkul umenikumbusha mbali sana
Marykimodo Jaman hata mi namkumbuka huyo jamaa

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE