January 24, 2015

Iraq yaendelea kukosoa harakati za kimaonyesho za Wamagharibi za kupambana na Daesh 
 Wawakilishi 35 wa bunge la nchini Iraq, ambao wanatilia shaka muungano wa kimataifa kwa ajili ya kupambana na kundi la kitakfiri na kigaidi la Daesh, wametaka kuundwa tume ya uchunguzi kwa ajili ya kufuatilia mwenendo wa muungano huo. Mwaka jana magaidi wa kitakfiri wa Daesh wanaoshirikiana na wanachama wa Kibaathi nchini humo, waliudhibiti mji wa Mosul ulioko katika mkoa wa Nainawa, baada ya kuushambulia mji huo. Baada ya kuudhibiti mji huo na miji mingine ya karibu, matakfiri hao walitekeleza vitendo vya kikatili na vya kutisha dhidi ya binaadamu. Moja ya vitendo hivyo ni ukatili dhidi ya watu wa jamii ndogo ya Kiyazidi nchini humo.
humo. Jinai za kundi hilo la Daesh zikiwemo zile za raia wa mji wa Kobani nchini Syria, ziliifanya Marekani ambayo mwaka 2011 iliondoa askari wake nchini Iraq, kwa mara nyingine ipate sababu ya kurejesha askari hao nchini humo kwa kisingizio cha eti kuwasaidia raia hao wachache wa Yazidi. Marekani kwa kushirikiana na zaidi ya nchi 40 waungaji mkono wake, iliunda muungano huo wa kimataifa dhidi ya kundi hilo la kitakfiri la Daesh ambalo lilianzishwa na Marekani yenyewe hapo mwezi Septemba mwaka jana. Licha ya kwamba Washington ilitangaza kuwa lengo la muungano huo ni kuendesha vita dhidi ya Daesh, lakini mienendo ya muungano huo wa kimataifa katika kipindi cha miezi minne iliyopita, inaonyesha kwamba lengo lake kuu si jingine ghairi ya kutekeleza njama zake nchini Iraq na Syria. Kwa upande mwingine ni kwamba, kutokana na Marekani na nchi za Magharibi kushindwa kuchukua hatua zozote za maana kuhusiana na jinai za wazi dhidi ya binaadamu, za kivita na zilizo dhidi ya usalama zilizotendwa na kundi hilo la kitafiri mbele ya vyombo vya sheria, nchi hizo zimejikuta chini ya mashinikizo makubwa. Ni kwa ajili hiyo, ndipo Marekani na waungaji mkono wake wa Kimagharibi sanjari na misaada ya udiplomasia wa dola zinazotokana na mafuta ya baadhi ya nchi za Kiarabu, wakaamua kuunda muungano huo wa kimaonyesho wa kimataifa dhidi ya kundi la Daesh, ili kwa njia hiyo waweze kupunguza mashinikizo ya walimwengu kuhusiana na kadhia hiyo. Aidha mbali na hapo ni kwamba, kwa kipindi chote cha miaka minne iliyopita Marekani na waungaji mkono wake wa Kimagharibi na Kiarabu, wamekuwa wakitoa uungaji mkono wa kila upande kwa makundi ya kigaidi nchini Syria, suala ambalo limetia wasi wasi mkubwa na kuilazimu serikali ya Rais Bashar al-Assad wa nchi hiyo kuzidisha mapambano dhidi ya makundi hayo ya kigaidi. Wasi wasi huo umeuondolea imani muungano huo wa kimataifa dhidi ya Daesh unaoongozwa na Marekani na kuwafanya watu waamini kwamba, lengo lake kuu ni kujaribu kulidhoofisha kwa muda mfupi tu kundi hilo na sio kuliangamiza kabisa. Ni kwa kuzingatia suala hilo, ndipo viongozi wa Iraq akiwemo Haider al-Abadi, Waziri Mkuu wa nchi hiyo wakakosoa mwenendo wa muungano uliotajwa, na kuamini kuwa mwendo wa muungano huo wa kimataifa dhidi ya Daesh ni kinyume na stratijia za serikali kuu ya Baghdad katika kukabiliana na kundi hilo la kigaidi. Matukio ya kiusalama nchini Iraq yanaonyesha kwamba, kudhoofika kwa makundi ya kigaidi nchini humo kumetokana na ushirikiano wa serikali ya nchi hiyo na wananchi, na wala sio mashambulizi ya muungano huo wa kimataifa unaoongozwa na Marekani. 

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE