December 18, 2014

Mwigizaji na mwongozaji wa filamu wa nchini Ghana, Van Vicker ameshangazwa na vyombo vya habari za udaku za hapa Bongo, kwa kile ambacho kimelipotiwa kuhusu yeye na muigizaji Wema Sepetu.
Kwenye blogs na magazeti mbalimbali ya udaku hapa Bongo zilijaa habari za kuwa Wema na Van Vicker mbali kucheza movie kuna mambo mambo walifanya eti kwa sababu tu Wema ameachana na aliekuwa mpenzi wake Diamond Platnumz na hivyo alitaka kumrusha roho, kitu ambacho hakina ukweli wowote.
Kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa INSTAGRAM, Van Vicker aliweka picha hiyo hapo juu na kui-caption
We are in the news in Tanzania...but the headline tho. Lol@wemasepetu
Akionyesha kuchekeshwa na vichwa vya habari zilizoenea hapa bongo kuhusu yeye na Wema.
Sasa sijui kuna watu wamemsomea mastori ya kutoka kwenye lile jumba kongwe la udaku hapa nchini.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE