December 18, 2014

 
STAA wa Bongo Fleva,Rehema Chalamila’’Ray C’ ameahirisha kuisambaza ngoma yake kwenye vituo vya redio kupisha msiba wa rafiki yake wa siku nyingi marehemu Aisha Madinda,ngoma hiyo inaitwa Nishum Shum tayari ipo kwenye mitandao.
Kupitia Instagram Ray C aliandika hivi...Nenda Dada yangu nenda! Nakumbuka tulikutana Kanisani Tabata ukanishuhudia Kwamba umeweza kuacha madawa ya kulevya na miguu yako imepona Kabisa kwa imani na mola na kwa maombezi ya nabii Joseph, nilipokuona ulivyokuwa umependeza nikajipa moyo huku nalia kwamba iko siku na mimi nitaacha madawa tulilia sana mimi na mama yangu pale Kanisani huku tukimwomba mungu aniokoe kwenye mateso yale, uliniangalia kwa huruMa wakati mimi na mama tunaondoka pale Kanisani ukamkimbilia mama na kumwomba namba yake huku ukimuahidi kuwa nitapona tu........Siku niliokutana na wewe tena mwananyamala hospitali ulinipita bila kunitambua nikakuita aisha? Ray C hapa ! Hukuamini macho yako kutakana na nilivyokuwa nimenenepa, tulicheka kwa furaha tukakumbushiana ya kanisani ukaniambia si nilikwambia utapona kwa uwezo wa mungu??? Nikamwambia natibiwa na methadone na wewe pia uko kitengo hichohicho muhimbili, tukaagana kwani nilikuwa nawahi kunywa dawa TUKAAGANA! NDIO SIKU YA MWISHO KUKUONA!Dada angu tangulia uniwekee na nafasi kwani najua lazma tutakuja onana tena mbele, ya haki, nimeshtuka sana ila najua mungu yuko nawe my sister, I will aways remember You DEAR.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE