November 19, 2014

 
NA SYLVESTER DAVID
MSANII mkongwe wa muziki wa kizazi kipya nchini kutoka katika kundi la ‘Wakali kwanza’,  Joslin Mchalla maarufu kama Joslin anatarajia kutambulisha kibao chake kipya hivi karibuni.

Akizungumza na MUZIKI BEGANI alisema amefanya kibao kizuri kitakachokonga nafsi za mashabiki wake.

“Nnimeamua kuandaa kibao hiki ambacho kitaamsha hisia za mashabiki ambao walikuwa wakinisubiri kwa muda mrefu kupata nyimbo kali kutoka kwangu”.Alisema Josline.

Joslin aliyewahi kutamba na vibao vikiwemo perfume,itika,niite basi na Tesa nae, alisema kwa sasa amejipanga vizuri kwa ajili ya wapenzi wa muziki wake.
Joslin aliongeza kuwa ameanza utaratibu wa kuachia nyimbo mpya  kila baada ya miezi minne ili kuwapa burudani zaidi mashabiki wake.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE