November 14, 2014

Tumeshasikia kuwa kuna msanii wa Marekani ambaye Diamond Platnumz tayari amefanya naye collabo ingawa bado hajamuweka wazi, lakini hivi karibuni alimtaja msanii mkubwa wa Mareknai ambaye ana ndoto ya kufanya naye pia collabo.



Akizungumza na show ya Sporah, Diamond amesema licha ya kufanikiwa kufanya collabo na baadhi ya wasanii wakubwa wa Africa kama Davido, Iyanya, Mafikizolo na wengine, lakini ndoto yake ya miaka mingi ni kufanya wimbo na hit maker wa ‘Good Kisser’, Usher Raymond.

“Natamani nifanye wimbo na Usher Raymond sana, natamani nifanye naye nyimbo kwasababu ni mtu ambaye nilikuwa nikimtazama tangia mdogo nakua, nikifanya nae nahisi nitatimiza moja ya ndoto zangu.” alisema.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE