November 24, 2014

CFP443948869-144059_copy1
‘Kumekuwa na taarifa katika vyombo vya habari na mitandaoni pia kwamba Serikali ilikuwa na mpango wa kuiondoa Jamii ya Wamasai katika eneo la Loliondo, ambapo Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu aliwahi kukanusha juu ya hilo siku tatu zilizopita.
Jana kupitia ukurasa wa Twitter, Rais Kikwete ameandika kwamba Serikali haina mpango na wala haitowatoa Wamasai kutoka katika ardhi hiyo ambayo ni urithi wa mababu wa jamii hiyo.
Ujumbe aliouandika Rais kupitia ukurasa wake wa Twitter jana Novemba 23 unasomeka hivi; “…There has never been, nor will there ever be any plan by the Government of to evict the people from their ancestral land…“– @jmkikwete
JK On Wamasai
Katika taarifa zilizoenea kwenye vyombo vya habari ilisemekana kuwa lengo la kuiondoa Jamii hiyo ni kuwapatia eneo lenye kilometa za mraba 1,500, kampuni ya OBC ya Falme za Kiarabu.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE