October 30, 2014


Tatizo la kukatika kwa umeme, imekuwa kero katika maeneo mbalimbali hapa nchini na lawama nyingi kutoka kwa wananchi zimekuwa zikielekezwa kwa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).
Maeneo mengi yamekumbwa na kero hiyo tangu wiki iliyopita mpaka jana huku wahusika wakishindwa kutoa taarifa ya nini kinachosababisha kero hiyo ya kukatika kwa umeme.
Hata hivyo Afisa habari wa TANESCO,Adrian Sevelin akizungumza na Clouds FM leo asubuhi alisema kuwa hali inatokana na matengenezo wanayofanya ikiwemo kubadilisha nguzo zilioza na kuweka nguzo mpya ili kukabiliana na kipindi cha mvua kinachokuja.
Ameongeza kuwa hakuna mgao wa umeme na katizo la umeme litaendelea hadi Nov.Mosi na ameomba radhi kwa wananchi kutokana na usumbufu uliojitokeza.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE