September 13, 2014

Nyumba ikiwa imeharibiwa na bomu,kama inavyoonekana
Mkutano kati ya waandishi habari na Waathirika wa Mabomu Mbagala, ambao umefanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mbagala Kuu ,jijini Dar-Es-Salaam mapema leo .
Waathirika hao wapatao 1,361 kati yao 25 wameishapoteza maisha kutokana na athari za mabomu hayo.
Mlipuko huo wa mabomu ni tukio lililotokea tarehe 29 April mwaka 2009,majira ya saa sita kasa robo katika eneo la mbagala kuu,hii ni baada ya mabomu hayo kulipuka katika ghala la silaha ya kambi ya ulinzi ya jeshi ya jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania(JWTZ) namba 671 kj.
Mabomu hayo yaliyokua yanalipuka kwa mfululizo yalisababisha vifo,kujeruhi,kuharibu makaazi na mali za watu kuharibiwa vibaya na kwa upande wa afya athari zilizojitokeza ni maradhi ya TB ama kifua kikuu,upofu wa macho,saratani,tezi yamkojo na kadhalika.
Leo hii wananchi wanadai kua serikali imewasahau na kuwatelekeza waathirika hao kiasi cha huduma za afya kukosekana,malazi kutorejea kama walivyoahidiwa na kila walipodai fidia wanapata majibu yasiyo faa ikiwemo, wanaoweza kusubiri wasubiri ama wasio kua na subira basi wajitoe.
Kwa mengi na undani wa habari hii ungana na AMKA NA BBFC JUMATATU uipate taarifa hii kwa utuo

Chanzo: bbswahili.com

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE