August 21, 2014

Screen Shot 2014-08-20 at 8.28.55 PM 

Mganda Emmanuel Okwi harudi tena Yanga na sasa ameweka wazi kwamba anashughulikia mipango yake kwenda kucheza soka la Ulaya >>> Okwi aachana na Yanga mchana kweupe!!!!! >>> Okwi achukizwa na ishu ya DVD ya Maximo <<<< hizo ni baadhi tu ya sentensi kwenye Magazeti mbalimbali ya Tanzania kwa wiki kadhaa ila ukweli kutoka kwa Okwi mwenyewe ni huu hapa chini.

Akiwa Kampala ameongea kwenye Exclusive interview na Bill the African ambae ni ripota wa millardayo.com na AyoTV Kampala Uganda na kusema haya >>> ‘Mimi na Yanga tulikua na makubaliano ya mkataba na hakuna ukweli kwamba Mshahara niliokua nalipwa Yanga ni mdogo, mshahara usingekua unatosha nisingekubali kusaini mkataba ‘ ‘Ni kweli kuna mambo mengi hayapo sawa kati yangu na club yangu ya Yanga ila ni mambo ya ndani ambayo nisingependa kuyazungumzia, ni mambo madogo ambayo nadhani yanaweza kuisha‘ ‘Hakuna ukweli kwamba mimi nakwenda Ulaya, sijui hata imetoka wapi na nani kaanzisha hii ya Ulaya, mimi bado ni mchezaji halali wa Yanga na huwa naongea nao karibu kila siku, hata jana nimetoka kuongea na katibu mkuu na mambo yote yanaelekea vizuri hamna shida yoyote mpaka sasa hivi‘
Kama unahitaji zaidi kupata ushahidi wa sauti yake Okwi akiongelea hi iishu bonyeza play hapa chin


Sas je wewe kama mdau unasemaje?? funguka

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE