July 23, 2014


Tukio la gari lilolobeba miili ya binadamu kukamatwa katika eneo la Bunju, Kinondoni, Dar es Salaam limevuta hisia za watu wengi huku jeshi la polisi likiwashikilia watu wanane wakiwemo madaktari wa hospitali ya IMTU.
Daktari wa IMTU ambaye hakutaka jina lake litajwe ameiambia Sunrise ya 100.5 Times kuwa kuna mtu ambaye alipewa kiasi cha shilingi milioni 4 ili akateketeze viungo hivyo na kwamba baada ya kulipwa pesa hiyo alifanya alichokijua tofauti na makubalino.
 “Kwa taarifa niliyonayo ingawa mimi sikumpa. Lakini kwa taarifa ni kwamba alipewa shilingi milioni 4 na akasema alienda kuviharibu. Kwa hiyo tulijua kwamba hiyo kazi ilitekelezwa vizuri kwa hiyo hatukuwa na wasiwasi wowote. Kumbe yeye badala ya kutumia hiyo hela kulipa maana kule Muhimbili wanalipa hela..” Amesema Daktari huyo.
Erick Martin, mtayarishaji wa kipindi cha Sunrise cha 100.5 Times Fm alimchimba daktari huyo kiudadisi akitaka kufahamu mtazamo wake kuhusu madaktari waliokamatwa kwa jinsi anavyolielewa tukio zima.
“Inaonekana miili ilitoka kwa hiyo bila shaka alipewa hiyo miili. Huenda sasa watu waliompa na hawa viongozi wa Muhimbili  wametiwa misukosuko naona wamelala rumande. Lakini mimi naona hawana kosa maana wamefanya kama inavyotakiwa, wao hawakujua kama viungo vitatupwa. Ila huenda kama walijua lakini sasa wanahojiwa na polisi na mimi siruhusiwi kuwepo au kuingilia…”
Amesema miili hiyo hupelekwa katika hospitali ambazo zinakifaa maalum cha kuteketeza bila kusababisha harufu yoyote na kwamba mtu aliyeamua kutupa wakati alilipwa alifanya fitina, “huyo aliyetupa alifanya kufuru yaani alifanya fitina.”
Daktari huyo ameeleza kuwa viungo hivyo vya miili ya binadamu hupatikana kutokana na miili ya marehemu ambao hawakutambulika na ndugu zao, lakini pia miili mingine hutolewa nje ya nchi ili kuondoa hali ya hisia za kuona viungo vya binadamu ambavyo ni vya watu wanaofahamika.
“Hizo maiti zinatumika kama vifaa vya kufundishia madaktari. Lakini hatuchukui maiti za hapa kwetu, tunachukua maiti kutoka nje ya nchi na za hapa ambazo labda kama zinapatikana zinapelekwa nchi zingine kwa ajili ya maadili. Haitakuwa vizuri kama mtu unaemfahamu kuona yuko huko anatumika kufundishia binadamu. Hiyo kutupa ndiyo imekosewa.” Ameeleza daktari huyo.
Amesema mbali na kupata maiti kutoka nje ya nchi, wapo watu wanaojitolea kama sadaka kuwa endapo watafariki  maiti zao zitumike kufundishia wanafunzi

Source: timesfm.co.tz

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE