April 17, 2014

 Helikopta inaonekana ikienda kusaidia  abiria 476  waliokuwamo kwenye meli ya Korea kusini iliyozama.
Helikopta inaonekana ikienda kusaidia abiria 476 waliokuwamo kwenye meli ya Korea kusini iliyozama.
 
Maafisa wa Korea kusini wanasema watu wanne wamefariki na wengine 290 hawajulikani walipo baada ya meli kuzama kwenye pwani ya kusini ya nchi hiyo Jumatano.

Meli hiyo ilikuwa na abiria zaidi ya 459 wengi wao walikuwa wanafunzi waliokuwa wakielekea kwenye kisiwa cha mapumziko cha Jeju,  ilizama katika wakati ambapo  hali baharini ilionekana kuwa ya utulivu.

Wengi wanahofiwa kuwa wamenasa ndani ya meli hiyo iliyozama au kukwama katika maeneo ya karibu ya majini ambayo ni ya kiasi cha joto la Celsius 12.

Dazeni ya helikopta na meli ikiwa ni pamoja na za jeshi la Marekani ikiwa ni pamoja na meli ya kijeshi ya Marekani Amphibia zinashiriki katika operesheni kubwa ya utafutaji na uokozi.
Kikosi cha wanajeshi wanamaji wa  Korea Kusini  “Navy Seal” wanatafuta meli hiyo iliyozama lakini maafisa wanaonya kuwa wale waliokwama ndani huenda wamepoteza maisha.

Walionusurika walipelekwa kwenye kisiwa cha karibu cha  Jindo.Kim Tae-young  mwanafunzi anasema alichukua hatua haraka wakati meli inaanza kuzama.

Abiria wengi wanasema mwanzo waliambiwa wabaki kwenye viti vyao wasijaribu kukimbia.Yoo Ho-shil anasema alipoona meli inaanza kuzama ilibidi achukue hatua haraka.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE