April 18, 2014


HALI ya kustaajabisha imetokea hivi karibuni katika msiba wa nguli wa muziki wa dansi, Muhidin Gurumo baada ya baadhi ya watu waliohudhuria kwenye mazishi hayo kufurahishwa na Nasibu Abdul ‘Diamond’ kutokuwepo kwenye shughuli hiyo. 
Msiba huo uliofanyika nyumbani kwa marehemu Mabibo jijini, ulihudhuriwa na watu wengi maarufu nchini lakini staa huyo wa wimbo wa My Number One hakuonekana eneo la tukio huku ikielezwa kuwa alibanwa na kazi zake za kimuziki. 
Kutokana na Diamond ambaye mwaka jana alimzawadia marehemu gari aina ya Fun Cargo, kutokuwepo kwake kulisababisha baadhi ya wahudhuriaji wasikike wakisema:

“Jamaa kama angekuja hapa kusingekuwa na msiba tena kwa sababu watu wote wangemfuata yeye na kutaka kuzungumza naye, kumzunguka muda wote kumsikia atakachokiongea, kwa hiyo ile hali ya watu kuwa msibani ingeondoka.” 

Mwingine akadakia: “Yaani afadhali hajaja na sijui hata kakwama wapi, kama angekuwepo hakuna kingine ambacho kingesikika na kuongeleka zaidi ya Diamond, sijui ana nini yule!”

Mjadala huo uliendelea muda mrefu huku kutokuwepo kwa msanii huyo kukifurahiwa na wengi. Baada ya kuondoka
nyumbani kwa nguli huyo mwili wake ulikwenda kuzikwa kwenye Makaburi ya Kijiji cha Masaki Kisarawe, Pwani.
  
Wakati wa shughuli ya kuuaga mwili wa Albert Mangwea kwenye Viwanja vya Leaders jijini, mwaka jana, kulitokea mvutano mkubwa baada ya Diamond kufika eneo la tukio lakini wakati alipotaka kuondoka alizungukwa na umati mkubwa jambo lililozua tafrani kubwa eneo hilo.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE