March 04, 2015

Watu 35 wafa kwa mafuriko

0 MAONI YAKO
 
Zaidi ya watu 35 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 55 wamejeruhiwa baada ya nyumba zao kuwaangukia na kuwafunika usiku wa kuamkia leo kutokana na mvua kubwa iliyonyesha wilayani Kahama, mkoani Shinyanga
  
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Benson Mpesya
Taarifa zilizothibitishwa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Benson Mpesya amesema mvua hiyo kubwa iliambatana na upepo mkali, hivyo nyumba nyingi zilianguka na nyingine kuezuliwa na kuharibiwa kabisa. Bw. Mpesya amesema hadi majira ya asubuhi walikuwa wamefanikiwa kupata miili ya watu 35 waliopoteza maisha baada ya kufukua nyumba nyingi, na majeruhi wamekimbizwa hospitali ya wilaya kwa matibabu.
Mkuu huyo wa Wilaya amesema nyumba nyingi zimeanguka na zoezi la kutafuta watu waliojeruhiwa au kupoteza maisha bado linaendelea kwa kasi.
Continue reading ...

Tanzania kukumbwa na ukame

0 MAONI YAKO
 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk.Agnes Kijazi (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam. 

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa taarifa ya mwelekeo wa mvua za masika katika kipindi cha Machi mpaka Mei na kusema kuwa hali ya mvua haitarajiwi kuwa ya kuridhisha katika maeneo mengi ya nchi.
TMA imesema kuwa kutokana na kuwapo kwa kiwango hicho cha mvua, maeneo mengi yatakumbwa na ukame.
Hayo yalisemwa jana na mkurugenzi mkuu wa TMA, Dk Agnes Kijazi alipokuwa akitoa mwelekeo wa hali ya hewa katika maeneo mengi ya nchi ambayo hayajapata mvua za masika za kutosha.
Aliitaja mikoa inayotarajiwa kupata mvua za wastani mpaka chini ya wastani kuwa ni Tanga, Pwani, Dar es Salaam, Unguja na Pemba, Morogoro, Kilimanjaro, Arusha na Simiyu.
Mikoa mingine ni Singida, Dodoma, Tabora, Katavi, Rukwa, Ruvuma, Lindi, Mtwara, Kigoma, Shinyanga na Manyara ambayo pia inatarajiwa kupata kiasi kidogo cha mvua.
Dk Kijazi alisema Kanda ya Ziwa inayohusisha mikoa ya Mwanza, Geita, Mara na Kagera inatarajiwa kupata mvua za wastani mpaka juu ya wastani.
Akizungumzia utabiri huo katika sekta ya kilimo, Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula, Karim Mtambo aliwataka wakulima wanaoishi katika maeneo yatakayopata mvua chini ya wastani kulima mazao yanayokomaa haraka na kustahamili ukame.
“Mikoa ya kanda ya Ziwa Victoria inaweza kupata mvua za wastani mpaka juu ya wastani, hivyo mamlaka husika zinapaswa kujiandaa kwa hali yoyote inayoweza kujitokeza,” alisema Dk Kijazi.
“Wasimamizi wa maeneo ya utalii wachukue hatua ya kuzuia uharibifu wa miundombinu ya barabara na madaraja katika mbuga zilizo karibu na maeneo ya Ziwa Victoria.”
Mtaalam wa Afya ya Jamii kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Jubilate Benard alisema kuna hatari ya kutokea kwa magonjwa ya mlipuko kwenye maeneo yatakayopata mvua nyingi.

Continue reading ...

Bajeti ya jeshi yaboreshwa China

0 MAONI YAKO
 
 China inasema kuwa bajeti yake ya ulinzi itaongezeka kwa asilimia kumi mwaka huu.
Wanajeshi wake wanatarajiwa kupewa dola bilioni 145 na kuendelea na mfumo wa kuongeza bajeti ya jeshi ulioanza miaka 20 iliyopita.
Taifa la Marekani ndilo hutumia fedha nyingi zaidi kwa bajeti ya jeshi.
Akitoa tangazo hilo msemaji wa serikali Fu Ying alisema kuwa China imejifunza kutokana na historia.
Japan nayo iliongeza bajeti ya jeshi lake mwaka huu baada ya kuipunguza kwa miaka mitatu mfululizo.
Continue reading ...

Kuhusu kauli ya Ngeleja kumtuhumu, Zitto Kabwe ataka achunguzwe

0 MAONI YAKO
 
Tuhuma dhidi yangu zichunguzwe-Zitto Kabwe
Katika kujitetea mbele ya Baraza la Maadili kuhusu tuhuma dhidi yake za kugawiwa mgawo wa fedha kutoka akaunti ya Escrow, mbunge wa Sengerema Bwana William Ngeleja alisema kuwa ni kawaida wabunge kupewa misaada na wafanyabiashara na taasisi za umma. Katika Maelezo yake alirudia tuhuma dhidi ya Mbunge wa Kigoma Zitto Kabwe, zitto aliwahi kupewa pesa . Sasa kupitia A/C ya Faceboopk Zitto amefunguka haya

1) nilipewa fedha na kampuni ya PAP na
2) nilipewa fedha na shirika la NSSF.

Tuhuma zote hizo nimewahi kuzitolea ufafanuzi na kukanusha kwani hazina msingi wowote na zilikuwa siasa za majitaka. Hata hivyo bado zimekuwa zikijirudia rudia kwa malengo maalumu wanayoyajua wanaotoa tuhuma hizo. Watuhumiwa wa ufisadi wa escrow hawajazoea kuona taasisi za maadili zikifanya kazi kwa namna ilivyo sasa na hivyo wanajaribu na watajaribu kubwabwaja na kuhangaika ikiwemo kutaka kila mtu aonekane ni mtuhumiwa kama wao. Ndio maana Bwana Ngeleja ametaja msururu wa watu wakiwemo wafanyabiashara kwamba huwapa fedha wabunge bila chembe ya ushahidi.
Hivyo narudia kutamka kwamba ninataka uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo ufanyike mara moja, wenye ushahidi wapeleke kwenye vyombo vya uchunguzi na niitwe mbele ya Baraza la Maadili kujieleza. Nikiwa mbunge ambaye maisha yangu yote ya siasa nimeyatumia kupambana na ufisadi na kuchochea mabadiliko ili kujenga misingi madhubuti ya uwajibikaji na kuimarisha taasisi zake, nipo tayari kwa uchunguzi mahususi dhidi yangu dhidi ya tuhuma zilizotolewa na nyingine zozote ambazo mtanzania yeyote anazo dhidi yangu.
Naunga Mkono kwa nguvu kubwa kazi inayofanywa na Baraza la Maadili. Ni kazi ambayo ilipaswa kuwa imefanyika kwa muda mrefu sana kwa kashfa mbali mbali ambazo viongozi wa umma wamepata kama vile ile ya rada, rushwa katika manunuzi ya mafuta mazito kuendesha mitambo ya Umeme, kujipatia mikopo kwenye taasisi za umma bila kulipa, kujilimbikizia Mali tofauti na kipato nk. Hivyo naiomba Sekretariat ya maadili iyachukue kwa uzito maoni ya Bwana Ngeleja na kama yana uzito kwa mujibu wa sheria na kanuni yafanyiwe uchunguzi. Nipo tayari kufanyiwa uchunguzi.
Katika kujenga Misingi Madhubuti ya uwajibikaji nchini ni lazima kila kiongozi aheshimu taasisi kama Baraza la Maadili. Baraza likiendelea kufanya kazi kama inavyofanyika sasa, vita dhidi ya ufisadi itakuwa imepiga hatua na porojo za kuzushiana mitaani zitapungua.
Zitto Kabwe
Mwenyekiti PAC
Dar Es salaam, tarehe 4 Machi 2015.

Continue reading ...

Mwizi wa wasanii Clouds huyu hapa

0 MAONI YAKO
 
Huyu kijana kushoto amekamatwa kwa kosa la kutapeli watu mbalimbali kwa kutumia majina ya wafanyakazi wa Clouds akiwemo Ruge Mutahaba na kujifanya yeye ndio kiongozi wa idara ya muziki ya Clouds fm na kuwatapeli wasanii chipukizi kwa kuomba rushwa ya hela ili nyimbo zao zichezwe redioni
Continue reading ...

Karibu hapa kuangalia Video mpya ya Fid Q inaitwa Bongo Hip Hop

0 MAONI YAKO
 Mkali wa Muziki wa Hip Hop toka Mwanza Tanzania Mkongwe Fareed Kubanda Fid Q hapa anakupa fursa ya kuitazama video ya wimbo wake uitwa Bongo Hip Hop

Bofya hapa Chini kutazma hii video na kisha weka Comment yako
       
Continue reading ...
 

COPYRIGHT © MACHAKU BLOG DESIGN BY DISMAS TEN 0713216125